Matendo 15:39-41 Biblia Habari Njema (BHN)

39. Basi, kukatokea ubishi mkali kati yao, wakaachana. Barnaba akamchukua Marko, wakapanda meli kwenda Kupro.

40. Naye Paulo akamchagua Sila, na baada ya ndugu wa mahali hapo kumweka chini ya ulinzi wa neema ya Bwana, akaondoka.

41. Katika safari hiyo alipitia Siria na Kilikia, akiyaimarisha makanisa.

Matendo 15