8. nao wawili watakuwa mwili mmoja. Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja.
9. Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asitenganishe.”
10. Walipoingia tena ndani ya nyumba, wanafunzi wake walimwuliza juu ya jambo hilo.
11. Naye akawaambia, “Anayemwacha mkewe na kuoa mwingine, anazini dhidi ya mkewe.
12. Na mwanamke anayemwacha mumewe na kuolewa na mwingine anazini.”
13. Watu walimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawakemea.