Luka 24:48-53 Biblia Habari Njema (BHN)

48. Nyinyi ni mashahidi wa mambo hayo.

49. Nami mwenyewe nitawapelekeeni yule ambaye Baba aliahidi kumtuma, lakini ngojeni huku mjini mpaka mtakapopewa ile nguvu itokayo juu.”

50. Kisha akawaongoza nje ya mji hadi Bethania, akainua mikono yake juu, akawabariki.

51. Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni.

52. Wao wakamwabudu, kisha wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha kubwa:

53. Wakakaa muda wote hekaluni wakimsifu Mungu.

Luka 24