Kutoka 40:4-7 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Utaiingiza meza na kupanga vyombo vyake juu. Utaingiza kile kinara pia na kuziweka taa zake juu yake.

5. Madhabahu ya dhahabu ya kufukizia ubani utaiweka mbele ya sanduku la ushuhuda, kisha utatundika pazia kwenye mlango wa hema takatifu.

6. Ile madhabahu ya kuteketezea sadaka utaiweka mbele ya mlango wa hema takatifu la mkutano.

7. Birika la kutawadhia utaliweka katikati ya hema la mkutano na madhabahu na kulijaza maji.

Kutoka 40