Kutoka 39:41-43 Biblia Habari Njema (BHN)

41. na mavazi yote yaliyofumwa vizuri kabisa kwa ajili ya huduma ya mahali patakatifu, yaani mavazi matakatifu ya kuhani Aroni, na ya wanawe kwa ajili ya huduma ya ukuhani.

42. Waisraeli walifanya kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

43. Mose alikagua kila kitu, akaridhika kwamba walikuwa wamefanya kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyoamuru. Hivyo Mose akawabariki.

Kutoka 39