Kutoka 33:17-23 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Kwa kuwa umepata fadhili mbele yangu, nami nakujua kwa jina lako, jambo hilihili ulilolisema nitalifanya.”

18. Mose akasema, “Nakusihi unioneshe utukufu wako.”

19. Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Nitapita mbele yako na kukuonesha wema wangu wote nikilitangaza jina langu, ‘Mwenyezi-Mungu’. Mimi nitamrehemu yule ninayependa kumrehemu, na kumhurumia yule ninayependa kumhurumia.

20. Lakini hutaweza kuniona uso maana hakuna mwanadamu yeyote atakayeniona na kuishi.”

21. Kisha Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Kuna mahali karibu nami ambapo utasimama juu ya mwamba;

22. na utukufu wangu utakapokuwa unapita, nitakutia katika pango mwambani na kukufunika kwa mkono wangu, mpaka nitakapokuwa nimepita.

23. Halafu nitauondoa mkono wangu nawe utaniona nyuma, lakini uso wangu hutauona.”

Kutoka 33