Kutoka 31:8-13 Biblia Habari Njema (BHN)

8. meza na vyombo vyake, kinara safi cha taa na vyombo vyake, madhabahu ya kufukizia ubani,

9. madhabahu ya sadaka za kuteketezwa na vyombo vyake vyote, birika la maji pamoja na tako lake,

10. mavazi matakatifu ya kuhani Aroni na wanawe ambao watafanya huduma ya ukuhani,

11. mafuta ya kupaka na ubani wenye harufu nzuri kwa ajili ya mahali patakatifu. Vitu hivyo vyote vitatengenezwa kulingana kabisa na jinsi nilivyokuamuru.”

12. Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose,

13. “Waambie Waisraeli hivi: Nyinyi mtaadhimisha Sabato zangu, kwa sababu hizo ni ishara kati yenu na mimi kwa vizazi vyote kwamba mimi ndimi ninayewatakasa.

Kutoka 31