Kutoka 21:11-15 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Iwapo huyo bwana hatamtimizia haki hizo tatu, basi, mke ataondoka na kuwa huru bila malipo yoyote.

12. “Ampigaye mtu na kumwua, lazima auawe.

13. Lakini kama hakuwa amemvizia, bali ni kwa ajali, basi, huyo mwuaji ataweza kukimbilia usalama mahali nitakapowachagulieni.

14. Lakini mtu akimshambulia mwenzake makusudi na kumwua kwa ujeuri, hata kama atakimbilia kwenye madhabahu, mtamtoa huko madhabahuni pangu na kumwua.

15. “Ampigaye baba yake au mama yake lazima auawe.

Kutoka 21