Kumbukumbu La Sheria 32:5-9 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Lakini nyinyi mmekosa uaminifu kwake,nyinyi sio watoto wake tena kwa sababu ya uovu,nyinyi ni kizazi kiovu na kipotovu.

6. Mnawezaje kumlipa hivyo Mwenyezi-Mungu,enyi watu wapumbavu na msio na akili?Je, yeye siye Baba yenu aliyewaumba,aliyewafanya na kuwaimarisha?

7. Kumbukeni siku zilizopita,fikirieni miaka ya vizazi vingi;waulizeni baba zenu nao watawajulisha,waulizeni wakubwa wenu nao watawaeleza.

8. Mungu Mkuu alipoyagawia mataifa mali yao,alipowagawa wanadamu,kila taifa alilipatia mipaka yake,

9. kulingana na idadi ya watoto wa Mungu,lakini alijiwekea watu wa Yakobo kuwa wake,hao alijichagulia kuwa mali yake.

Kumbukumbu La Sheria 32