Kumbukumbu La Sheria 23:22-25 Biblia Habari Njema (BHN)

22. Lakini ukiacha kuweka nadhiri hutakuwa na dhambi.

23. Uwe mwangalifu kutimiza nadhiri uliyotamka kwa mdomo wako, maana ulimwahidi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, kwa hiari yako.

24. “Ukipitia katika shamba la mzabibu la jirani yako unaweza kula zabibu kadiri uwezavyo, lakini usichume na kuchukua zabibu zozote kikapuni mwako.

25. Ukipitia katika shamba la jirani yako lenye nafaka unaweza kukwanyua masuke kwa mkono na kula, lakini usichukue mundu kukata mazao yake.

Kumbukumbu La Sheria 23