3. Wewe, ee Mungu, umelikuza taifa,umeiongeza furaha yake.Watu wanafurahi mbele yako,wana furaha kama wakati wa mavuno,kama wafurahivyo wanaogawana nyara.
4. Maana nira nzito walizobeba,nira walizokuwa wamefungwa,na fimbo ya wanyapara wao,umezivunjavunja kama wakati wa Wamidiani.
5. Viatu vyote vya washambulizi vitanina mavazi yote yenye madoa ya damuyatateketezwa kama kuni za kuwasha moto.
6. Maana mtoto amezaliwa kwa ajili yetu,tumepewa mtoto wa kiume.Naye atapewa mamlaka ya kutawala.Ataitwa: “Mshauri wa Ajabu”.“Mungu Mwenye Nguvu”,“Baba wa Milele”,“Mfalme wa Amani”.
7. Utawala wake utastawi daima,amani ya ufalme wake haitakoma.Atachukua wadhifa wa mfalme Daudina kutawala juu ya ufalme wake;ataustawisha na kuuimarisha,kwa haki na uadilifu,tangu sasa na hata milele.Hayo atayafanya Mwenyezi-Mungu wa majeshi.