Isaya 9:11-18 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Basi, Mwenyezi-Mungu atawaletea wapinzanina kuwachochea maadui zao.

12. Waaramu upande wa mashariki,Wafilisti upande wa magharibi,wamepanua vinywa vyao kuimeza Israeli.Hata hivyo, hasira yake haijatulia,bado ameunyosha mkono wake.

13. Ingawa aliwaadhibu watu,hawakumrudia Mwenyezi-Mungu wa majeshi.

14. Basi kwa muda wa siku moja tu,Mwenyezi-Mungu atakata katika Israeli vichwa na mikia,tawi la mtende na nyasi:

15. Vichwa ndio wazee na waheshimiwa,mikia ndio manabii wafundishao uongo.

16. Wale wanaoongoza watu hawa wamewapotosha,na hao wanaoongozwa nao wamepotoka.

17. Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu hawahurumii vijana wao,hana huruma juu ya yatima na wajane wao;kwani hakuna hata mmoja amchaye Mungu,kila mtu husema uongo.Hata hivyo, hasira yake haijatulia,bado ameunyosha mkono wake.

18. Uovu huwaka kama motouteketezao mbigili na miiba;huwaka kama moto msituni,na kutoa moshi mzito upandao angani juu.

Isaya 9