Isaya 54:5-10 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Muumba wako atakuwa mume wako;Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ndilo jina lake,Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako;yeye aitwa ‘Mungu wa ulimwengu wote’.

6. “Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu amekuita tena wewekama vile mke aliyeachwa na kuhuzunika,mke aliyeolewa akiwa kijana akaachwa.Mungu wako anasema:

7. Nilikuacha kwa muda mfupi tu;kwa huruma nyingi, nitakurudisha.

8. Kwa hasira nyingi nilikuficha uso wangu kwa kitambo,lakini kwa fadhili za milele nitakuonea huruma.Mimi Mwenyezi-Mungu Mkombozi wako, nimesema.

9. “Nitafanya kama nilivyofanya wakati wa Noa:Wakati ule niliapa kwambasitaifunika tena ardhi kwa gharika.Basi sasa naapa kwamba sitakukasirikia tenawala sitakukemea tena.

10. Milima yaweza kutoweka,vilima vyaweza kuondolewa,lakini fadhili zangu hazitakuondoka,agano langu la amani halitaondolewa.Mimi Mwenyezi-Mungu nikuhurumiaye nimesema.

Isaya 54