Isaya 52:2-7 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Jikungute mavumbi, uinukeewe Yerusalemu uliyetekwa nyara!Jifungue minyororo yako shingoni,ewe binti Siyoni uliyechukuliwa mateka.

3. Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nyinyi mliuzwa utumwani bila malipo yoyote, na mtakombolewa bila kulipa hata senti moja.

4. Tena mwanzoni nyinyi watu wangu mlikimbilia Misri mkakaa huko. Halafu baadaye Waashuru waliwakandamiza bila sababu yoyote.

5. Katika hali ya sasa napata faida gani kuwaona watu wangu wamepelekwa utumwani? Hao wanaowatawala wanajitapa. Nalo jina langu laendelea kudharauliwa kila siku.

6. Kwa hiyo watu wangu watajua mimi ni nani; siku hiyo watajua kwamba ni mimi ninayesema: Niko!”

7. Tazama inavyopendezakumwona mjumbe akitokea mlimani,ambaye anatangaza amani,ambaye analeta habari njema,na kutangaza ukombozi!Anauambia mji wa Siyoni:“Mungu wako anatawala!”

Isaya 52