Isaya 45:15-20 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Kweli wewe ni Mungu uliyefichika,Mungu wa Israeli, Mungu Mwokozi.

16. Watengenezaji sanamu wataaibika na kufadhaika,wote kwa pamoja watavurugika.

17. Lakini taifa la Israeli litaokolewa na Mwenyezi-Mungu,litapata wokovu wa milele.Halitaaibishwa wala kufadhaishwa milele.

18. Mwenyezi-Mungu, Mungu pekee,ndiye aliyeiumba dunia,ndiye aliyeiumba na kuitegemeza.Hakuiumba iwe ghasia na tupu,ila aliiumba ikaliwe na viumbe vyake.Yeye asema sasa:“Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu,wala hakuna mwingine.

19. Mimi sikunena kwa siri,wala katika nchi yenye giza.Mimi sikuwaambia wazawa wa Yakobowanitafute katika ghasia.Mimi Mwenyezi-Mungu husema ukweli,maneno yangu ni ya kuaminika.”

20. Enyi watu wa mataifa mliosalia,kusanyikeni pamoja mje!Nyinyi mmekosa akili:Nyinyi mwabeba sanamu za mitina kumwomba mungu asiyeweza kuokoa watu.

Isaya 45