14. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Utajiri wa Misri na bidhaa za Kushi,pamoja na za watu wa Seba, majitu marefu,zitakuja kwako mwenyewe wewe taifa la Israeli,zote zitakuwa mali yako.Watu hao watakutumikia wamefungwa minyororo;watakusujudia na kukiri wakisema:‘Kwako kuna Mungu wa kweli,wala hakuna Mungu mwingine ila yeye.’”
15. Kweli wewe ni Mungu uliyefichika,Mungu wa Israeli, Mungu Mwokozi.
16. Watengenezaji sanamu wataaibika na kufadhaika,wote kwa pamoja watavurugika.
17. Lakini taifa la Israeli litaokolewa na Mwenyezi-Mungu,litapata wokovu wa milele.Halitaaibishwa wala kufadhaishwa milele.
18. Mwenyezi-Mungu, Mungu pekee,ndiye aliyeiumba dunia,ndiye aliyeiumba na kuitegemeza.Hakuiumba iwe ghasia na tupu,ila aliiumba ikaliwe na viumbe vyake.Yeye asema sasa:“Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu,wala hakuna mwingine.