Isaya 38:7-13 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Isaya akamjibu, “Hii itakuwa ishara kwako kutoka kwa Mwenyezi-Mungu kwamba Mwenyezi-Mungu atafanya kama alivyoahidi.

8. Nitafanya kivuli kwenye ngazi iliyojengwa na Ahazi, kirudi nyuma hatua kumi.” Nacho kivuli kikarudi nyuma hatua kumi.

9. Kisha mfalme Hezekia alipopona, akatunga wimbo huu wa shukrani:

10. “Nilisema: Nikiwa mbichi kabisa,inanibidi niage dunia.Mimi nimepangiwa kwenda kuzimusiku zote zilizonibakia.

11. Nilisema sitamwona tena Mwenyezi-Mungu,katika nchi ya walio hai;wala sitamwona mtu yeyote tena,miongoni mwa wakazi wa ulimwengu.

12. Makao yangu yamengolewa kwangu,kama hema la mchungaji;kama, mfumanguo nimefungasha maisha yangu;Mungu amenikatilia mbali;kabla hata mwisho wa siku amenikomesha.

13. Usiku kucha nililia kuomba msaada;kama simba, anavunjavunja mifupa yangu;mchana na usiku ananikomesha.

Isaya 38