Isaya 34:6-10 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Upanga utalowa damu na kutapakaa mafuta,kama kwa damu ya kondoo na mbuzi,na mafuta ya figo za kondoo dume.Maana Mwenyezi-Mungu atatoa kafara huko Bosra,kutakuwa na mauaji makubwa nchini Edomu.

7. Nyati wataangamia pamoja nao,ndama kadhalika na mafahali.Nchi italoweshwa damu,udongo utarutubika kwa mafuta yao.

8. Maana Mwenyezi-Mungu anayo siku ya kisasi;mwaka wa kulipiza maadui wa Siyoni.

9. Vijito vya Edomu vitatiririka lami,udongo wake utakuwa madini ya kiberiti;ardhi yake itakuwa lami iwakayo.

10. Itawaka usiku na mchana bila kuzimika,moshi wake utafuka juu milele.Nchi itakuwa jangwa siku zote,hakuna atakayepitia huko milele.

Isaya 34