Isaya 30:17-25 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Watu wenu elfu moja watamkimbia askari mmoja adui;na askari watano maadui watawakimbizeni nyote.Mwishowe, watakaosaliawatakuwa kama mlingoti wa bendera mlimani,kama alama iliyo juu ya kilima.

18. Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu anangoja awafadhili,atainuka na kuwaonea huruma.Maana, Mwenyezi-Mungu ni Mungu atendaye haki.Heri wote wale wanaomtumainia.

19. Enyi watu wa Siyoni, enyi watu wa Yerusalemu, hakika nyinyi hamtaomboleza tena. Kweli Mungu atawahurumia; mara tu atakaposikia kilio chenu atawaitikeni.

20. Ingawa Bwana atawalisha taabu na kuwanywesha dhiki, yeye ndiye Mwalimu wenu na hatajificha tena; nanyi mtamwona kwa macho yenu wenyewe.

21. Mkienda kulia au kushoto, mtasikia sauti nyuma yenu ikisema, “Njia ni hii; ifuateni.”

22. Mtavifanya haramu vinyago vyenu vya miungu vilivyopakwa fedha na sanamu zenu zilizopakwa dhahabu. Mtazitupilia mbali kama vitu najisi, mkisema, “Poteleeni mbali!”

23. Mtakapopanda mbegu zenu, Mwenyezi-Mungu atanyesha mvua kwa wakati wake, nazo zitakua na kuwapa mavuno mengi. Mifugo yenu nayo itapata malisho kwa wingi.

24. Mafahali na punda wenu wa kulimia watapata malisho yaliyochambuliwa vizuri na kutiwa chumvi.

25. Wakati utakapofika ambapo maadui watauawa na ngome zao kubomolewa, vijito vya maji vitatiririka kutoka kila mlima na kilima.

Isaya 30