1. Sasa, Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshiataondoa kutoka Yerusalemu na Yuda kila tegemeo:Tegemeo lote la chakula,na tegemeo lote la kinywaji.
2. Ataondoa mashujaa na askari,waamuzi na manabii,waaguzi na wazee,
3. majemadari wa vikosi vya watu hamsini,na watu wenye vyeo,washauri, wachawi stadi na walozi hodari.