1. Siku ile watu wataimba wimbo huu katika nchi ya Yuda:Sisi tuna mji imara:Mungu anatulinda kwa kuta na ngome.
2. Fungueni malango ya mji,taifa aminifu liingie;taifa litendalo mambo ya haki.
3. Ee Mungu, wawaweka katika amani walio thabiti,wawaweka katika amani kwa kuwa wanakutegemea.
4. Mtumaini Mwenyezi-Mungu siku zotekwa maana yeye ni mwamba wa usalama milele.
5. Amewaporomosha waliokaa pande za juu,mji maarufu ameuangusha mpaka chini,ameutupa mpaka mavumbini.