Isaya 21:14-17 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Enyi wakazi wa nchi ya Tema,wapeni maji hao wenye kiu;wapelekeeni chakula hao wakimbizi.

15. Maana wamekimbia mapanga,mapanga yaliyochomolewa,pinde zilizovutwa na ukali wa mapigano.

16. Maana Bwana aliniambia hivi: “Katika muda wa mwaka mmoja, bila kuzidi wala kupungua, fahari yote ya Kedari itakwisha.

17. Wapiga upinde wachache kati ya mashujaa wa watu wa Kedari ndio watakaosalia. Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nimenena.”

Isaya 21