1. Kauli ya Mungu dhidi ya nchi ya Misri.“Mwenyezi-Mungu amepanda juu ya wingu liendalo kasina kuja mpaka nchi ya Misri.Sanamu za miungu ya Wamisri zitatetemeka mbele yake,mioyo ya Wamisri itayeyuka kwa hofu.
2. Mimi nitawachochea Wamisri wagongane:Ndugu na ndugu yake,jirani na jirani yake,mji mmoja na mji mwingine,mfalme mmoja na mfalme mwingine.
3. Nitawaondolea Wamisri uhodari wao,nitaivuruga mipango yao;watatafuta maoni kwa sanamu na mizimu,wachawi, mizuka na pepo.
4. Nitawatia Wamisri mikononi mwa bwana katili,mfalme mkali ambaye atawatawala.Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nimenena.”
5. Maji ya mto Nili yatakaushwa,nao utakauka kabisa.
6. Mifereji yake itatoa uvundo,vijito vyake vitapunguka na kukauka.Nyasi na mafunjo yake yataoza.
7. Sehemu za kandokando ya Nili zitakuwa tupu.Mimea yote iliyopandwa humo itakaukana kupeperushiwa mbali na kutoweka.