Hosea 8:4-10 Biblia Habari Njema (BHN)

4. “Walijiwekea wafalme bila kibali changu,walijiteulia viongozi ambao sikuwatambua.Wamejitengenezea miungu ya fedha na dhahabu,jambo ambalo litawaangamiza.

5. Watu wa Samaria, naichukia sanamu yenu ya ndama.Hasira yangu inawaka dhidi yenu.Mtaendelea mpaka lini kuwa na hatia?

6. Nanyi Waisraeli ni hivyohivyo!Na sanamu yenu hiyo fundi ndiye aliyeitengeneza.Yenyewe si Mungu hata kidogo.Naam! Sanamu ya ndama ya Samaria itavunjwavunjwa!

7. “Wanapanda upepo, watavuna kimbunga!Mimea yao ya nafaka iliyo mashambanihaitatoa nafaka yoyote.Na hata kama ikizaa,mazao yake yataliwa na wageni.

8. Waisraeli wamemezwa;sasa wamo kati ya mataifa mengine,kama chombo kisicho na faida yoyote;

9. kwa kuwa wamekwenda kuomba msaada Ashuru.Efraimu ni punda anayetangatanga peke yake;Efraimu amekodisha wapenzi wake.

10. Wametafuta wapenzi kati ya watu wa mataifa,lakini mimi nitawakusanya mara.Na hapo watasikia uzito wa mzigo,ambao mfalme wa wakuu aliwatwika.

Hosea 8