Hosea 8:2-5 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Waisraeli hunililia wakisema:‘Mungu wetu, sisi tunakujua.’

3. Lakini Israeli amepuuza mambo mema,kwa hiyo, sasa adui watamfuatia.

4. “Walijiwekea wafalme bila kibali changu,walijiteulia viongozi ambao sikuwatambua.Wamejitengenezea miungu ya fedha na dhahabu,jambo ambalo litawaangamiza.

5. Watu wa Samaria, naichukia sanamu yenu ya ndama.Hasira yangu inawaka dhidi yenu.Mtaendelea mpaka lini kuwa na hatia?

Hosea 8