4. Yakobo akiwa bado tumboni mwa mama yake,alimshika kisigino kaka yake.Na alipokuwa mtu mzimaalishindana na Mungu.
5. Alipambana na malaika, akamshinda;alilia machozi na kuomba ahurumiwe.Huko Betheli, alikutana na Mungu,huko Mungu aliongea naye.
6. Mwenyezi-Mungu, wa majeshi,Mwenyezi-Mungu, ndilo jina lake.Lakini nyinyi mrudieni Mungu wenu.Zingatieni upendo na haki,mtumainieni Mungu wenu daima.
7. “Efraimu ni sawa na mfanyabiasharaatumiaye mizani danganyifu,apendaye kudhulumu watu.
8. Efraimu amesema,‘Mimi ni tajiri!Mimi nimejitajirisha!Hamna ubaya kupata faida.Hata hivyo, hilo si kosa!’”