44. kisahani kimoja cha dhahabu cha gramu 110 kikiwa kimejazwa ubani;
45. fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
46. beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi;
47. na mafahali wawili, beberu watano, na wanakondoo madume watano wa mwaka mmoja kwa ajili ya tambiko ya sadaka za amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Eliasafu mwana wa Deuli.
48. Siku ya saba ikawa zamu ya Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa kabila la Efraimu.