17. Kisha Mwenyezi-Mungu akawaambia Mose na Aroni,
18. “Msiache ukoo wa familia za Kohathi miongoni mwa Walawi uangamizwe.
19. Basi, ili kuwaepusha wasije wakauawa kwa kuvikaribia vyombo hivyo vitakatifu sana utafanya hivi: Aroni na wanawe wataingia na kumpangia kila mmoja wao wajibu wake na kazi yake.
20. Lakini wazawa wa Kohathi hawataingia kamwe kuvitazama vitu hivyo vitakatifu sana; wakifanya hivyo watakufa.”
21. Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose,
22. “Wahesabu watu wa ukoo wa Gershoni, kufuatana na familia na koo zao;
23. utawahesabu wanaume wote wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini wanaofaa kujiunga na huduma ya hema la mkutano.
24. Wajibu wao utakuwa huu: Watabeba mapazia ya hema takatifu na hema la mkutano pamoja na