Hesabu 36:8-12 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Mwanamke yeyote mwenye urithi katika kabila mojawapo la Israeli ni lazima aolewe na mtu wa kabila lake, ili kila Mwisraeli achukue urithi wa babu zake.

9. Hivyo hapatakuwa na urithi wowote utakaohamishwa kutoka kabila moja hadi jingine. Kila kabila la Waisraeli litashikilia urithi wake.”

10. Binti za Selofehadi walifanya kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

11. Wote: Mala, Tirza, Hogla, Milka na Noa wakaolewa na binamu zao.

12. Waliolewa katika jamaa za ukoo wa Manase mwana wa Yosefu, na urithi wao ukabaki katika kabila la baba yao.

Hesabu 36