Hesabu 34:14-23 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Kabila la Reubeni na la Gadi, na nusu ya kabila la Manase yamepata urithi wao kulingana na koo zao.

15. Makabila hayo mawili na nusu yamepata urithi wao ngambo ya mto Yordani upande wa mashariki, mkabala wa Yeriko, mawioni.”

16. Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose,

17. “Kuhani Eleazari na Yoshua mwana wa Nuni ndio watakaowagawia watu nchi kuwa mali yao.

18. Utachukua pia kiongozi mmoja kutoka kila kabila kusaidia katika ugawaji wa nchi.

19. Haya ndiyo majina yao:Kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune.

20. Kabila la Simeoni, Shemueli mwana wa Amihudi.

21. Kabila la Benyamini, Elidadi mwana wa Kisloni.

22. Kabila la Dani, Buki mwana wa Yogli.

23. Kabila la Manase mwanawe Yosefu, Hanieli mwana wa Efodi.

Hesabu 34