6. Kutoka Sukothi, walipiga kambi yao huko Ethamu, ukingoni mwa jangwa.
7. Kutoka Ethamu, waligeuka na kurudi hadi Pi-hahirothi, mashariki ya Baal-sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli.
8. Waliondoka Pi-hahirothi, wakapita bahari ya Shamu mpaka jangwa la Ethamu; walisafiri jangwani mwendo wa siku tatu, wakapiga kambi yao Mara.
9. Kutoka Mara, walisafiri hadi Elimu; huko Elimu kulikuwa na chemchemi kumi na mbili za maji na mitende sabini, wakapiga kambi yao mahali hapo.
10. Walisafiri kutoka Elimu, wakapiga kambi yao karibu na bahari ya Shamu.
11. Kutoka Bahari ya Shamu walipiga kambi yao katika jangwa la Sini.
12. Kutoka jangwa la Sini, walipiga kambi yao Dofka.
13. Kutoka Dofka walipiga kambi yao huko Alushi.
14. Kutoka Alushi walipiga kambi yao huko Refidimu, ambapo hapakuwa na maji ya kunywa.
15. Waliondoka Refidimu wakapiga kambi yao katika jangwa la Sinai.
16. Kutoka Sinai walipiga kambi yao huko Kibroth-hataava.
17. Kutoka Kibroth-hataava, walipiga kambi yao huko Haserothi.
18. Kutoka Haserothi, walipiga kambi yao huko Rithma.
19. Kutoka Rithma, walipiga kambi yao huko Rimon-perezi.
20. Kutoka Rimon-perezi, walipiga kambi yao huko Libna.
21. Kutoka Libna walipiga kambi yao Risa.
22. Waliondoka Risa, wakapiga kambi yao huko Kehelatha.
23. Kutoka Kehelatha, walipiga kambi yao kwenye Mlima Sheferi.
24. Kutoka Mlima Sheferi walipiga kambi yao huko Harada.
25. Kutoka Harada, walipiga kambi yao huko Makelothi.