21. Kisha Balaamu akawaangalia Wakeni, akatoa kauli hii:“Makao yenu ni salama, enyi Wakeni,kama kiota juu kabisa mwambani.
22. Lakini mtateketezwa, enyi Wakeni.Mtachukuliwa mateka na Ashuru mpaka lini?”
23. Tena Balaamu akatoa kauli hii:“Lo! Nani ataishi, Mungu atakapofanya hayo?
24. Meli zitafika kutoka Kitimu,wataishambulia Ashuru na Eberi,lakini nao pia wataangamia milele.”
25. Basi, Balaamu akaondoka, akarudi nyumbani; Balaki pia akaenda zake.