Hesabu 2:9-21 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Jumla yote ya watu watakaokuwa katika kambi ya Yuda kulingana na makundi yao ni watu 186,400. Hao ndio watakaotangulia kusafiri.

10. “Kwa upande wa kusini, wale walio chini ya bendera ya kundi la Reubeni kulingana na makundi yao, kiongozi wao akiwa Elisuri mwana wa Shedeuri,

11. kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 46,500.

12. Kisha wale watakaopiga kambi kando ya watu wa Reubeni watakuwa ni watu wa kabila la Simeoni, kiongozi wao akiwa Shelumieli mwana wa Suri-shadai,

13. kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 59,300.

14. Hatimaye kabila la Gadi, kiongozi wao akiwa Eliasafu mwana wa Reueli,

15. kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 45,650.

16. Jumla ya wanaume watakaokuwa katika kambi ya Reubeni kulingana na makundi yao ni watu 151,450. Hawa ndio watakaokuwa katika msafara wa pili.

17. “Halafu, kambi ya kabila la Walawi, ikiwa katikati ya kambi zote, na wakiwa wamebeba hilo hema la mkutano, wataondoka; kila kundi litasafiri kwa kufuata nafasi yake chini ya bendera yao.

18. “Kwa upande wa magharibi, wale walio chini ya bendera ya kundi la Efraimu watapiga kambi kulingana na makundi yao, kiongozi wao akiwa Elishama mwana wa Amihudi,

19. kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 32,200.

20. Mara tu baada ya Waefraimu litafuata kabila la Manase: Kiongozi wake akiwa Gamalieli, mwana wa Pedasuri,

21. kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa watu 32,000.

Hesabu 2