Hesabu 2:17-25 Biblia Habari Njema (BHN)

17. “Halafu, kambi ya kabila la Walawi, ikiwa katikati ya kambi zote, na wakiwa wamebeba hilo hema la mkutano, wataondoka; kila kundi litasafiri kwa kufuata nafasi yake chini ya bendera yao.

18. “Kwa upande wa magharibi, wale walio chini ya bendera ya kundi la Efraimu watapiga kambi kulingana na makundi yao, kiongozi wao akiwa Elishama mwana wa Amihudi,

19. kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 32,200.

20. Mara tu baada ya Waefraimu litafuata kabila la Manase: Kiongozi wake akiwa Gamalieli, mwana wa Pedasuri,

21. kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa watu 32,000.

22. Hatimaye kabila la Benyamini: Kiongozi wake ni Abidani, mwana wa Gideoni,

23. kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 35,400.

24. Jumla ya watu watakaokuwa katika kambi ya Efraimu kulingana na makundi yao ni watu 108,100. Kundi hili la Efraimu litakuwa katika msafara wa tatu.

25. “Kwa upande wa kaskazini, watapiga kambi katika makundi yao wale walio chini ya bendera ya Dani, kiongozi wao atakuwa Ahiezeri, mwana wa Amishadai,

Hesabu 2