1. Mwenyezi-Mungu aliwapa Mose na Aroni, maagizo yafuatayo:
2. “Waisraeli watapiga kambi zao, kila mmoja akikaa mahali penye bendera yake, penye alama za ukoo wake. Watapiga kambi zao kulizunguka hema la mkutano.
3. “Wale watakaopiga kambi upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua watakuwa kikundi cha watu walio chini ya bendera ya Yuda na kiongozi wao atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu,
4. kikosi chake kulingana na hesabu ni wanaume 74600.
5. Wale watakaofuata kupiga kambi baada ya watu wa Yuda watakuwa kabila la Isakari, kiongozi wao akiwa Nethaneli mwana wa Suari,
6. kikosi chake kulingana na hesabu ni wanaume 54,400.
7. Kisha kabila la Zebuluni, kiongozi wao akiwa Eliabu mwana wa Heloni,
8. kikosi chake kulingana na hesabu ni wanaume 57,400.
9. Jumla yote ya watu watakaokuwa katika kambi ya Yuda kulingana na makundi yao ni watu 186,400. Hao ndio watakaotangulia kusafiri.
10. “Kwa upande wa kusini, wale walio chini ya bendera ya kundi la Reubeni kulingana na makundi yao, kiongozi wao akiwa Elisuri mwana wa Shedeuri,
11. kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 46,500.
12. Kisha wale watakaopiga kambi kando ya watu wa Reubeni watakuwa ni watu wa kabila la Simeoni, kiongozi wao akiwa Shelumieli mwana wa Suri-shadai,
13. kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 59,300.
14. Hatimaye kabila la Gadi, kiongozi wao akiwa Eliasafu mwana wa Reueli,