Hesabu 17:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose,

2. “Waambie Waisraeli wakuletee fimbo kumi na mbili, kila kiongozi wa kabila fimbo moja. Liandike jina la kila mmoja wao kwenye fimbo yake,

3. na jina la Aroni liandike juu ya fimbo inayowakilisha kabila la Lawi. Patakuwa na fimbo moja kwa kila kiongozi wa kabila.

4. Zichukue fimbo hizo katika hema la mkutano na kuziweka mbele ya sanduku la agano, mahali ambapo mimi hukutana nawe.

5. Fimbo ya mtu nitakayemchagua itachipua. Kwa njia hii nitayakomesha manunguniko ya Waisraeli juu yenu.”

6. Mose akaongea na watu wa Israeli. Viongozi wao wote wakampa kila mmoja fimbo yake kulingana na kabila lake jumla zikawa fimbo kumi na mbili. Fimbo ya Aroni iliwekwa pamoja na fimbo hizo.

7. Mose akaziweka fimbo hizo zote mbele ya Mwenyezi-Mungu katika hema la mkutano.

Hesabu 17