Hesabu 1:3-14 Biblia Habari Njema (BHN)

3. wale wote katika Israeli wanaoweza kwenda vitani, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, mtawaweka katika orodha ya vikosi vikosi.

4. Tena mwanamume mmoja wa kila kabila atakuwa pamoja nanyi, kila mmoja aliye kiongozi wa jamaa za kabila lake.

5. Haya ndiyo majina ya watu watakaokusaidia:Kabila la Reubeni: Elisuri, mwana wa Shedeuri;

6. Kabila la Simeoni: Shelumieli mwana wa Suri-shadai;

7. Kabila la Yuda: Nashoni mwana wa Aminadabu;

8. Kabila la Isakari: Nethaneli mwana wa Suari;

9. Kabila la Zebuluni: Eliabu mwana wa Heloni;

10. Kabila la Efraimu: Elishama mwana wa Amihudi;Kabila la Manase: Gamalieli mwana wa Pedasuri;

11. Kabila la Benyamini: Abidani mwana wa Gideoni;

12. Kabila la Dani: Ahiezeri mwana wa Amishadai;

13. Kabila la Asheri: Pagieli mwana wa Okrani;

14. Kabila la Gadi: Eliasafu mwana wa Deueli;

Hesabu 1