Hesabu 1:2-20 Biblia Habari Njema (BHN)

2. “Wewe na Aroni fanyeni sensa ya jumuiya yote ya Waisraeli, familia mojamoja kwa kufuata koo zao na idadi ya majina yao kila mwanamume mmojammoja;

3. wale wote katika Israeli wanaoweza kwenda vitani, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, mtawaweka katika orodha ya vikosi vikosi.

4. Tena mwanamume mmoja wa kila kabila atakuwa pamoja nanyi, kila mmoja aliye kiongozi wa jamaa za kabila lake.

5. Haya ndiyo majina ya watu watakaokusaidia:Kabila la Reubeni: Elisuri, mwana wa Shedeuri;

6. Kabila la Simeoni: Shelumieli mwana wa Suri-shadai;

7. Kabila la Yuda: Nashoni mwana wa Aminadabu;

8. Kabila la Isakari: Nethaneli mwana wa Suari;

9. Kabila la Zebuluni: Eliabu mwana wa Heloni;

10. Kabila la Efraimu: Elishama mwana wa Amihudi;Kabila la Manase: Gamalieli mwana wa Pedasuri;

11. Kabila la Benyamini: Abidani mwana wa Gideoni;

12. Kabila la Dani: Ahiezeri mwana wa Amishadai;

13. Kabila la Asheri: Pagieli mwana wa Okrani;

14. Kabila la Gadi: Eliasafu mwana wa Deueli;

15. Kabila la Naftali: Ahira mwana wa Enani.”

16. Hawa ndio viongozi waliochaguliwa miongoni mwa jumuiya yote ya watu wa Israeli, kama viongozi wakuu wa makabila yao na viongozi wa koo za Israeli.

17. Basi, Mose na Aroni wakawachukua watu hawa waliotajwa,

18. na mnamo siku ya kwanza ya mwezi wa pili, wakaikusanya jumuiya yote ya watu waliokuwa wamehesabiwa kila mmoja kulingana na familia yake na ukoo wake. Kufuatana na majina ya watu waliokuwa na umri wa miaka ishirini na zaidi, mmojammoja,

19. kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. Mose akawahesabu watu hawa kule jangwani Sinai.

20. Watu waliotoka katika kabila la Reubeni aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Israeli, kwa kufuata vizazi vyao, kulingana na familia zao na jamaa zao, kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, kila mwanamume aliyekuwa na umri wa miaka ishirini na zaidi, aliyefaa kuingia jeshini,

Hesabu 1