15. Kwa farasi wako ulitembea juu ya bahari,bahari inayosukwasukwa na mawimbi.
16. Nasikia hayo nami ninashtuka mwilini,midomo yangu inatetemeka kwa hofu;mifupa yangu inateguka,miguu yangu inatetemeka.Ninangojea kwa utulivu siku ile ya maafa,ambayo inawajia wale wanaotushambulia.
17. Hata kama mitini isipochanua maua,wala mizabibu kuzaa zabibu;hata kama mizeituni isipozaa zeituni,na mashamba yasipotoa chakula;hata kama kondoo wakitoweka zizini,na mifugo kukosekana mazizini,
18. mimi nitaendelea kumfurahia Mwenyezi-Mungunitamshangilia Mungu anayeniokoa.
19. Bwana, Mwenyezi-Mungu ndiye nguvu yangu,huiimarisha miguu yangu kama ya paa,huniwezesha kupita juu milimani.