1. Mimi nitasimama mahali pa kuchungulia,na kukaa juu mnarani;nitakaa macho nione ataniambia nini,atajibu nini kuhusu lalamiko langu.”
2. Kisha, Mwenyezi-Mungu akanijibu hivi:“Yaandike maono haya;yaandike wazi juu ya vibao,anayepitia hapo apate kuyasoma.