Filemoni 1:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mimi Paulo, mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu, na ndugu Timotheo, ninakuandikia wewe Filemoni mpendwa, mfanyakazi mwenzetu,

2. na kanisa linalokutana nyumbani kwako, na wewe dada Afia, na askari mwenzetu Arkipo.

3. Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.

4. Kila wakati ninaposali, nakukumbuka wewe Filemoni, na kumshukuru Mungu,

5. maana nasikia habari za imani yako kwa Bwana Yesu na upendo wako kwa watu wote wa Mungu.

6. Naomba ili imani hiyo unayoshiriki pamoja nasi ikuwezeshe kuwa na ujuzi mkamilifu zaidi wa baraka zote tunazopata katika kuungana kwetu na Kristo.

7. Ndugu, upendo wako umeniletea furaha kubwa na kunipa moyo sana! Nawe umeichangamsha mioyo ya watu wa Mungu.

8. Kwa sababu hiyo, ningeweza, kwa uhodari kabisa, nikiwa ndugu yako katika kuungana na Kristo, kukuamuru ufanye unachopaswa kufanya.

9. Lakini kwa sababu ya upendo, ni afadhali zaidi nikuombe. Nafanya hivi ingawa mimi ni Paulo, balozi wa Kristo Yesu, na sasa pia mfungwa kwa ajili yake.

Filemoni 1