9. Sitawaachilia wala sitawaonea huruma.Nitawaadhibu kulingana na mienendo yenumaadamu machukizo yapo bado miongoni mwenu.Ndipo mtakapotambua kuwa ni mimi Mwenyezi-Mungu ninayewaangamiza.
10. “Tazameni, siku ile inakuja!Maangamizi yenu yamekuja.Ukatili uko kila mahali na kiburi kimechanua.
11. Ukatili unaendelea kuwa mbaya zaidi.Hakuna hata mmoja wenu atakayebaki,wala vitu mlivyojirundikia kwa wingi au utajiri wenu;hatakuwako mtu mwenye heshima miongoni mwenu.