Ezekieli 42:3-8 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Kulikuwako ghorofa tatu zilizounganisha mita 10 za ua wa ndani na zikiwa mkabala wa sakafu ya ua wa nje.

4. Upande wa kaskazini wa jengo hilo, kulikuwa na njia ya kupitia yenye upana wa mita 5 na urefu wake mita 50. Milango yake ilikuwa upande wa kaskazini.

5. Vyumba vya juu vilikuwa vyembamba kuliko vile vya katikati na vya chini kwani vilikuwa mbali zaidi.

6. Vile vyumba vya juu kabisa vilijengwa kwenye miinuko na havikusaidiwa na nguzo kama majengo mengine kwenye ua wa nje.

7. Kulikuwa na ukuta mkabala na vyumba kuelekea uwanja wa nje ukiwa na urefu wa mita 25.

8. Wakati vyumba kwenye ua wa nje vikiwa na urefu wa mita 20, vile vya mkabala na hekalu vilikuwa na urefu wa mita 50.

Ezekieli 42