Ezekieli 39:2-5 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Nitakugeuza na kukuelekeza upande mwingine na kukuongoza kutoka mbali kaskazini uende kushambulia milima ya Israeli.

3. Kisha nitauvunja upinde wako katika mkono wako wa kushoto, na mishale yako katika mkono wako wa kulia nitaiangusha chini.

4. Utakufa juu ya milima ya Israeli, wewe pamoja na vikosi vyako vyote na mataifa yaliyo pamoja nawe. Nami nitaitoa miili yao iliwe na ndege wa kila aina na wanyama wakali.

5. Utafia porini. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Ezekieli 39