Ezekieli 32:19-22 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Waambie:Nyinyi ni wazuri kuliko nani?Nendeni kuzimu mlazwe pamoja na wasiomjua Mungu!

20. Watu wa Misri wataangamia pamoja na watu waliouawa vitani. Upanga uko tayari kuangamiza Misri pamoja na watu wake wengi.

21. Wakuu wenye nguvu pamoja na wasaidizi wao wakiwa huko shimoni kwa wafu watasema hivi: ‘Wamisri wameshuka chini kwa wafu, wanalala pamoja na watu wasiomjua Mungu, waliouawa vitani.’

22. “Waashuru wako huko, wamezungukwa na makaburi ya wanajeshi wao. Wote waliuawa vitani,

Ezekieli 32