15. “Nitakapoifanya nchi ya Misri kuwa jangwa na mali yake yote kuchukuliwa, nitakapowaua wakazi wake wote, ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.
16. “Huo ndio utenzi wa maombolezo,wanawake wa mataifa watauimba,wataimba juu ya Misri na watu wake wote.Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nimesema.”
17. Siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, mwaka wa kumi na mbili tangu kuhamishwa kwetu, neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia: