1. Mnamo siku ya kwanza ya mwezi wa tatu, mwaka wa kumi na moja tangu uhamisho wetu, neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:
2. “Wewe mtu! Mwambie hivi Farao mfalme wa Misri na watu wake wote:Wewe wafanana na nini kwa ukuu wako?
3. Wewe ni kama mwerezi wa Lebanoniwenye matawi mazuri na majani mengi na shina refu.Kilele chake kinafika hata mawinguni.
4. Maji yaliustawisha,vilindi vya maji viliulisha.Mito ilibubujika mahali ulipoota,ikapeleka vijito kwenye miti yote ya msituni.