Ezekieli 26:7-11 Biblia Habari Njema (BHN)

7. “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kutoka kaskazini nitamleta Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, mfalme wa wafalme, akiwa na farasi, magari ya vita, wapandafarasi na jeshi kubwa, aje kukushambulia.

8. Ataiangamiza miji iliyo jirani nawe huko bara. Kisha atajenga kuta za kukushambulia, atajaza udongo kwenye kuta zako na kuweka ukuta wenye ngao ili kukushambulia.

9. Ataweka magogo yake ya kubomolea mbele ya kuta zako, na kwa mitalimbo ataivunjilia mbali minara yako.

10. Farasi wa mfalme Nebukadneza ni wengi na vumbi watakalotimua litakufunika. Kuta zako zitatetemeka kwa mshindo wa wapandafarasi na magari ya vita na ya mizigo wakati atakapoingia kwenye malango yako kama watu waingiavyo mjini kupitia mahali palipobomolewa.

11. Kwa kwato za farasi wake, ataikanyaga mitaa yako yote. Atawaua watu wako kwa panga; minara yako mikubwa ataiangusha chini.

Ezekieli 26