Ezekieli 26:17-21 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Wataimba utenzi huu wa kuomboleza:Umeangamizwa wewe mji maarufu,umetoweka kutoka baharini!Wakazi wake walieneza nguvu zao juu ya bahari,ambapo walihofiwa na wote.

18. Sasa watu wa bara wanatetemekakwa sababu ya kuanguka kwake;wakazi wa pwani, wametishika kwa kutoweka kwako!

19. “Maana, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitakufanya wewe Tiro kuwa mahame, kama miji isiyo na watu, nitakapoleta juu yako maji kutoka vilindi vya bahari, na maji mengi yatakufunika.

20. Nitakuteremsha shimoni ili ujiunge na walioko huko, walioishi duniani zamani; nitakufanya ukae huko katika mahame milele. Hutakaliwa na watu milele na hutakuwa na nafasi miongoni mwa nchi za walio hai.

21. Nitakufanya kuwa kitisho wala hutakuwapo tena; watu watakutafuta, lakini hawatakupata tena. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Ezekieli 26