Ezekieli 24:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mnamo siku ya kumi, mwezi wa kumi, mwaka wa tisa tangu kuhamishwa kwetu, neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:

2. “Wewe mtu! Andika tarehe ya siku ya leo, maana hii ni siku ambapo mfalme wa Babuloni anaanza kuuzingira mji wa Yerusalemu.

3. Wape mfano hao watu wangu waasi na kuwaambia kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema:Kiweke chungu juu ya meko,ukakijaze maji pia.

4. Tia humo vipande vya nyama,vipande vizuri vya mapaja na mabega.Kijaze pia mifupa mizuri.

5. Tumia nyama nzuri ya kondoo,panga kuni chini ya chungu,chemsha vipande vya nyama na mifupa,vyote uvichemshe vizuri.

Ezekieli 24